Friday, November 16, 2007

Gavana wa Georgia aomba mvua - Mungu ajibu

A Drying Lake in Georgia
Governor Sonny Perdue and his wife pray for Rain

Siku ya jumanne wiki hii watu walimcheka Gavana Sonny Perdue, wa Georgia alivyongoza mamia ya watu kuomba mvua kwenye maombi maalum mbele ya Ikulu ya huko mjini Atlanta. Walivyokuwa wanaomba kulikuwa hakuna dalili ya mvua hata kidogo! Siku hiyo ya jumanne watu walilamika kwa nini Gavana analeta mambo ya dini hapo! Walisema anatia aibu.

Jumatano na jana alhamisi, Mungu alijibu na kuwapa mvua. Mvua eneyewe haitoshi kumaliza ukame mbaya huko lakini itasaidia. Sasa sijui waliokuwa wanamcheka na kumsanifu wanasemaje sasa. Mungu yupo! Nani anacheka sasa?

Kama hamjasikia huko kusini mwa Marekani kuna ukame mbaya sana mabayo haijawaji kutokea. Kwa sasa kuna vizuizi kwenye matumizi ya maji huko. Wanasema kuwa bila mvua wamebakiza maji ya kutosha siku chache tu.

Wengi wenu mnafahamu waMarekani hawajazoea shida, kama kukosa maji au umeme.

Kwa habari zaidi someni:




1 comment:

Anonymous said...

Kweli Mungu yupo. Bwana Asifiwe sana. AMEN.