Tuesday, November 20, 2007

Huko New Jersey sasa ruksa kula Maskwereli!


Kama uko Marekani lazima umeona hao wanyama wadogo wadogo wenye mikia mirefu. Wana vichwa kama sungura lakini wana masikio madogo. Wanakimbia haraka haraka. Wako kila sehemu ambako kuna miti. Na kutegemeana na sehemu unayokaa unaweza kuwaona wenye rangi nyesusi, wekundu au wenye rangi ya kijivu. Hao wanyama ni watundu na wajanja.

Kuna wakati niliweka bird feeder kwenye balcony. Ndege walikuwa wanakuja kula. Sasa kuna siku nilitazama na kuona squirrel anahomoa chakula cha ndege akiwa kichwa chini miguu juu. Nilishangaa alifikaje maana feeder enyewe ilikuwa inaing'inia katikati ya balcony. Kumbe aliruka kutoka kwenye mti karibu na pale! DOH!

Kumbe hapa Marekani hao wanyama walikuwa wanaliwa kama kuku! Tuseme siku hizi kwa vile watu wanapata chakula supermarkets wamesahau chakula cha mababu zao na sasa wanaona hao squirrels kama pets. Nimeona sinema kadhaa za historia ya Marekani na watu walikuwa wanatafuta squirrels. Vijana wadogo walikuwa mafundi wa kuwakamata. Na walisifia nyama yao kuwa ni laini.

Juzi umati wa waMarekani walikumbushwa kuwa wanaliwa mkoa wa New Jersey walipotangaza kuwa wanafaa kuliwa. Kwanza walisema kuwa watu wasile eti wana vipande vya vyuma. Sasa wamesema wako safi kabisa kuliwa!

Hivyo usisahanagae ukialikwa kula squirrel stew!

******************************************************************************

Good news for New Jersey squirrel eaters

NEW YORK (AFP) - Squirrel eaters in the US state of New Jersey have been told that the bushy-tailed rodents are likely safe to eat, after earlier being advised the unlikely delicacies could contain toxic metals.
The Environmental Protection Agency said earlier this year it had discovered high levels of lead in a squirrel taken from near a waste dump in the Ringwood area and advised people to eat the rodents no more than twice a week.

Officials have now said the test results were an error.

"A blender that was used to process the tissues into usable samples was defective and was identified as the source of the lead contamination," the Environmental Protection Agency said in a statement dated Monday.

The New Jersey Division of Fish and Wildlife describes squirrel as "good table fare," offering recipes for squirrel chowder, stew and barbecue.

3 comments:

Anonymous said...

CHEMI HAO KWA KISWAHILI CHA HUKU ZNZ TUNAWAITA CHINDI. INAONEKANA HUJUI KWA KISWAHILI WANAITWAJE.

HEBU TAMKA "CHINDI" WAINGEREZA NDIO HUWAITA SQUIRREL

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 9:39AM, asante kwa maelezo. Hata sikujua kama wako ZNZ. Sijawaona bara.

Anonymous said...

The government is trying to curb the squirrel population by getting people to eat them. Their skins actually make good fur coats.